KUFUATIA
kutokea kwa vurugu kubwa jana katika mechi yabkimataifa ya kombe la
Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe na kupelekea kupigwa kwa mabomu
ya machozi na kutumika kwa maji ya kuwasha Kamishna msaidizi wa Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Temeke (ACP), Gilles Muroto amesema kuwa jana
vikosi vya usalama viliweza kutumia njia hizo kwa ajili ya kutuliza
ghasia zilizosababishwa na mashabiki wa mpira waliotaka kuingia ndani na
kuzuiliwa kuingia uwanjani.
Akizungumza
na Mtandao huu, amesema kuwa walikamata watu takribani watu 20 lakini
wameshawaachia kwani walifanya hivyo kwa ajili ya usalama wao na zaidi
hawakuwa pale kwa kwa lengo wa kuwakamata bali ni kulinda amani.
"Tulikuwa
pale kwa ajili ya kulinda amani na zaidi tuliwakata vijana 20 na
tumewaachia tayari kwani tulifanya hivyo kwa kulinda usalama wao kwani
vurugu zilikuwa nyingi sana, ila kazi kubwa ilifanywa na vikosi vya
usalama na wamefanya kazi kubwa sana,"amesema Muroto. Kwa mara ya kwanza
uwanja wa Taifa umeweza kuchukua watu wengi zaidi tofauti na idadi
inayohitajika na kwa hali hiyo ilikuwa ni hatari sana pale unapozidisha
watu,
Katika
mechi hiyo, watu waliweza kujitokeza uwanjani kuanzia majira ya saa 11
alfajiri na kitu kama hicgo hakijawahi kutokea na hata wale mateja
pamoja na vibaka walikuwa wengi sana na lazima nguvu ya ziada itumike
hasa baada ya wananchi kuvamia geti na kuliangusha na kuanza kuingia
ndani kwa nguvu kitu kilichopelekea kuanza kutumia mabomu ya machozi na
maji ya kuwasha.
Uongozi
wa Yanga uliwatangazia mashabiki wa soka kuwa hakutakuwa na kiingilio
katika mechi yao ambapo maelfu ya watu walikuja kwa wingi na kuweka
maswali kwa jamii watu hao wote hawana ajira au waliamua kutokwenda
kwenye kazi zao kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo ambayo ilikuwa
katikati ya wiki ila hali ya ndani ya uwanja ilikuwa tulivu na amani.
Sign up here with your email


