Akizungumza na gazeti hili, Cathy
alisema tangu mumewe ahamie kikazi Zanzibar maneno yamekuwa mengi sana
kutoka kwa watu wake wa karibu kwamba ameachwa kitu ambacho siyo kweli
kwani wako vizuri na mambo yao ya kifamilia yanakwenda vizuri.
“Nawashangaa sana wanaonisengenya kwamba
nimeachwa, jamani siwezi kuachwa na mume wangu kamwe ila tumekuwa mbali
kwa sababu tu ya kazi maana alihamishiwa Zanzibar na mimi nikabaki huku
Dar ili kuendeleza miradi yetu mingine maana tungehamia wote huko
tungepoteza vitu vyetu vingi vya maendeleo,” alisema Cathy bila kuwataja
majina ‘wabaya’ wake.
Sign up here with your email
