Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpang.
Stori: Gladness Mallya, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Baada ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe
Magufuli (JPM) kupitia kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango
kusoma bajeti yake kwa mwaka 2016/17 ya shilingi trilioni 29.5, mastaa
mbalimbali na wasanii wa filamu na muziki Bongo, wametoa ya moyoni
kuhusiana na bajeti hiyo:
“Kiukweli serikali ingeangalia vizuri
kwa sababu kama ingetaka kuongeza mapato, isingeongeza kodi ya kusajili
magari kwa majina binafsi mara mbili kutoka shilingi milioni tano hadi
10 kama walivyofanya. Pia kwenye usajili wa magari wasingeongeza kutoka
shilingi 150,000 hadi 250,000.
“Kwa upande wangu naona bajeti haipo
sawa na haijaangalia wananchi kwani ukitaka kumbadilisha mtu
usimbadilishe mpaka akahisi anatoka damu.”
“Unajua muwamba ngoma siku zote huvutia
kwake, wasanii wanaomiliki magari ni wachache sana na naona kupandishwa
kwa gharama za umiliki ni kitu kidogo sana.
“Nafurahi kwa sababu bajeti imetuangalia
sana wasanii kwa kutengewa bilioni tatu, ni jambo zuri kwani
itatunufaisha sana wasanii. Kuhusu magari, hizo ni starehe tu cha muhimu
ni sanaa yetu isonge mbele ikishaenda mbele hayo mengine yote
yatakuja.”
JACOB STEPHEN ‘JB’ (MUIGIZAJI)
“Kilichonifurahisha kwenye bajeti ni
suala la kudhibiti filamu za nje zinazoingia kinyemela, pia naiomba
serikali itumie hizo bilioni tatu kwa ajili ya kudhibiti wezi wa kazi
zetu maana ndiyo kilio kikubwa kwetu.
“Wasanii hawana tatizo la fedha za
kucheza filamu bali tatizo kubwa ni wezi na soko linaloeleweka kwa jumla
maana sekta ya sanaa inaajiri watu wengi kuliko sekta yoyote hivyo
iangaliwe kwa makini zaidi. Kuhusu magari na vinywaji hizo ni starehe tu
tena ingewezekana vingepandishwa bei zaidi ya hapo.”
“Kiukweli serikali inabidi iwatazame
watu inaowatengea hiyo bajeti kwa maana inajua kabisa kilio cha kila
mwananchi sasa hivi ni pesa kuwa adimu.
“Pia usafiri ni sekta muhimu sana katika
kukuza uchumi wa nchi na mwananchi mmojammoja kwa sababu sekta hii
ndiyo mahususi katika kusafirisha watu na mizigo kwa hiyo inavyopandisha
gharama za umiliki na usajili itapunguza uwezekano wa watu kumiliki
vyombo vya usafiri.
“Inaweza pia kuathiri pato la taifa
maana kwenye usafiri huongeza pato la taifa kutokana na kodi, shughuli
za walipa kodi zinazotegemea usafirishaji, bajeti hii naona ina madhara
makubwa kuliko faida.”
“Yaani naunga mkono bajeti iko safi sana.”
“Bajeti ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania 2016/2017, kwa upande wangu naona ipo vizuri sana
kwa sababu ukiangalia jinsi hizo trilioni 29.5 za bajeti
zilivyogawanywa, utagundua kwamba mambo yote ya msingi yamepewa
kipaumbele hasa utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo uliopewa asilimia
40 ya fedha zote.
“Hii ni dira ya kuonesha tunaelekea wapi
na naamini nchi itapiga hatua kuanzia kwenye uchumi, elimu, huduma za
kijamii, utalii na sanaa kwa jumla.
Sign up here with your email
