Sheikh Hemed Jalala akizungumza na
wanahabari wakati wa maadhimisho ya Siku ya QUDS ndani ya Msikiti wa
Kigogo Post jijini Dar es Salaam.
Wakati waumini wa dini ya Kiislam duniani na nchini Tanzania
wakiendelea na mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, wito umetolewa kwa
viongozi wa kidini pamoja na vyombo vya umoja wa mataifa kuhakikisha
kuwa wanarudisha hali ya amani katika nchi ya Palestina ambayo wananchi
wake wamekuwa wakiishi katika mateso, dhuluma na hali ngumu kutoka kwa
nchi ya Israeli na kuwafanya wananchi wa hao kushindwa kufurahia kuishi
katika nchi yao.Wito huo umetolewa na Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia nchini Tanzania kutoka Msikiti wa Kigogo Post uliopo jijini Dar es Salaam, Sheikh Hemed Jalala wakati wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya QUADS duniani ambayo ni siku inayotumika kuwakumbuka na kutafakari kwa pamoja mateso na mambo mbaya wanayopitia wananchi wa Palestina.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kislam wakipata semina juu ya siku hiyo ya QUDS katika Msikiti wa Kigogo Post Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari, Sheikh Jalala amesema kuwa Wapalestina
wamezagaaa duniani kwa kufukuzwa katika nchi yao na kuishi kwa mateso
ambapo amesema kuwa wao kama Waislam hawawezi kukubali uvamizi kama huu
kwa watu ambao hawana hatia hivyo wanaomba vyombo vinavyohusika vikiwemo
vile vya umoja wa mataifa kuhakikisha wanarudisha amani kama iliyopo
Tanzania kwani uwezo wa kufanya hivyo upo.Ameeleza kuwa kwa mtu ambaye anatambua historia ya nchi hiyo ya Palestina na mambo yanayopitia ni dhuluma, ukandamizaji na mateso makubwa jambo ambalo halifai kunyamaziwa, huku akisema kuwa ni ukweli kwamba mambo ya Palestina ni ya Wapalestina ila kwa sasa Palestina haipo mikononi mwa Wapalestina jambo ambalo linawapa nguvu wao kuinuka na kupiga kelele juu ya wanadamu hao wanaoteseka bila hatia.
Itakumbukwa kuwa mgogoro wa nchi hizo mbili kati ya Israel na Palestina umekuwa wa muda mrefu huku ukisahaulika ambapo wananchi wa Palestina wamekuwa wakikumbana na mateso makubwa kutoka kwa majeshi ya Israel na hata wengine kuikimbia nchi hiyo kutokana na mateso hayo jambo ambalo limekuwa likiwanyanyua vinywa viongozi wa dini mbalimbali akiwemo Sheikh Jalala kulaani mateso hayo yanayoendelea nchini humo.
Sign up here with your email