Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo kimewapa raha Watanzania baada ya kuichapa timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Shelisheli mabao 3-0.
Mechi hiyo ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika imepigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano kati ya timu hizo utapigwa Julai 2, mwaka huu nchini Shelisheli.
Sign up here with your email