Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza kuwa katika utawala wake
hatateua mbunge kuwa mkuu wa Mkoa au Wilaya. Amesema lengo ni kuboresha
utendaji kazi na uwajibikaji, kwamba "Haiwezekani katika watanzania mil.
50 tukose watu hadi turundie watu vyeo.
Tunataka tuchape kazi kwa ufanisi na ufanisi hauwezi kuja kwa kumrundikia mtu vyeo"