Diwani
wa kata ya Miono ,wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ,Juma Mpwimbwi
,akizungumzia juu ya tatizo la njaa katika baadhi ya maeneo ya kata
hiyo kwa mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete ,aliye kushoto
kwa diwani huyo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
NA Mwamvua Mwinyi
DIWANI
wa kata ya Mioni ,jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
,Juma Mpwimbwi amemuomba mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete ,kuvalia
njuga tatizo la njaa ambalo limewakumba baadhi ya wananchi katika kata
hiyo.
Amesema
kwasasa hali ni ngumu hususan katika vijiji vya Masimbani na Kwaikonje
ambapo ni miaka mitatu mfululizo sasa hawana chakula huku misimu ya
kilimo ikiwa imebadilika hivyo hawana hata vibarua vya kulima .
Mpwimbwi amemuomba mbunge huyo kusimamia suala hilo ili kunusuru familia ambazo zinaishi kwa shida bila chakula.
Akizungumza
juzi,mbele ya mbunge wa jimbo hilo,pamoja na baadhi ya wananchi katika
kata hiyo, Mpwimbwi alisema uhaba wa chakula upo zaidi maeneo ya
pembezoni mwa kata .
“Ni
afadhali ya sisi tunaoishi hapa mjini mjini maana mtu anaweza akamwomba
mwenzie hata sembe ama kuuza mkaa wake kwa sh.1,500 kwa kiroba cha kilo
25 licha ya kuzoeleka kuuza mkaa huo kwa sh.5,000”
"Imefikia
hatua nawakimbia watu,mtu akija kuniulizia nyumbani kwangu inabidi
waambiwe sipo,kwakuwa mimi mwenye hela ya kusaidia watu wote sina na
najisikia vibaya kuona mtu ananifuata halafu nimwambia hela ama chakula
cha kumpa sina"alisema Mpwimbwi.
Nae
Ridhiwani alisema anatambua tatizo hilo linalowakabili wakazi hao na
kusema taarifa tayari ipo kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa na wakati
wowote kuanzia sasa chakula cha msaaada kitapelekwa kwa walengwa.
Alieleza
kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita aliongea na waziri mkuu ambapo
alimwambia kuwa katibu tawala mkoa(RAS)ameshapeleka taarifa yake ya
uhakiki ambapo kwa wilaya ya Bagamoyo mahitaji ya chakula yanayotakiwa
ni tani 4,369.
Hata
hivyo Ridhiwani alisema hivi karibuni viongozi na watendaji wa vijiji
wote walipewa agizo la kuhakikisha wanaandika mahitaji ya chakula na
kisha kuipeleka ngazi ya wilaya ,mkoa na kwa waziri mkuu.
“Kila
zama na kitabu chake ,inabidi tukubaliane na hili kwani ilitakiwa
kujiridhisha na taarifa zilizotolewa kabla ya kufanya maamuzi ili
kuepukana na tatizo lililokuwepo zamani la baadhi ya watendaji kuzidisha
tani 5 kumbe ni tani mbili za chakula “
“Lakini
hatua zinachukuliwa kwani taarifa zilishakwenda kwa waziri mkuu
akaagiza kufanyika uhakiki kwanza kwa wilaya kujiridhisha na taarifa
huku uhakiki ukionyesha kuwa ni tani 4,369 zinazohitajika
kiwilaya”alisema Ridhiwani.
Sign up here with your email