NDANDA FC KUTAJA SILAHA WAKATI WOWOTE. - Rhevan Media

NDANDA FC KUTAJA SILAHA WAKATI WOWOTE.



TIMU ya soka ya Ndanda ya mkoani Mtwara, inatarajiwa kuanika usajili wake muda mfupi kutoka sasa baada ya baadhi ya mambo ya usajili kukamilika.
Akizungumza na DIMBA jana, Ofisa habari wa timu hiyo, Idris Bandari, alisema ripoti ya benchi lao la ufundi iliwataka kusajili wachezaji 10 jambo ambalo wanaendelea kulifanyia kazi.
“Ripoti ya kocha wetu ilituelekeza kusajili wachezaji 10, hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani dhamira yetu ni kumpatia kocha kile anachokihitaji.
“Usajili huo umelenga kuhakikisha msimu ujao tunakuwa na kikosi bora kitakacholeta ushindani na kwa kuzingatia hilo tumeongeza damu changa na wakongwe,” alisema.
Alisema katika usajili huo wa wachezaji 10, watano kati yao ni kutoka timu yao ya vijana baada ya kuridhishwa na uwezo wao.
Previous
Next Post »