MH .RAIS MAGUFULI AONGEA HAYA JUU YA ILANI YA CCM. - Rhevan Media

MH .RAIS MAGUFULI AONGEA HAYA JUU YA ILANI YA CCM.

Kwa heshima na Taadhima napenda kumkumbusha Rais Magufuli kuwa, nchi yoyote duniani inaongozwa kwa Katiba ya nchi husika, na sio Ilani ya Chama. Ilani ya Chama hutumika tu kuomba ridhaa ya wananchi (kura), ili Chama husika kipate kupewa Mamlaka ya kuongoza nchi, chini ya Katiba.

Kuzuia vyama vya Siasa hasa vya Upinzani kuendesha shughuli zake za kisiasa, kwa kisingizio cha kukwamisha ahadi za Ilani ya Chama Chako CCM, ni hatua hatari sana ya kutokufuata Katiba ya nchi, ambayo ndio sheria mama inayoongoza nchi.

Kumbuka Ilani ya CCM haiwezi kuwa mbadala wa Katiba ya Nchi. Na madikteta wote duniani hupuuza Katiba.

Nakuomba na Kukusihi kwa jina la Mwenyezi Mungu, uongeze nchi kwa mujibu wa Katiba, ili usije ukaingia kwenye kumbukumbu za madikteta wa Dunia.

Nawasilisha.
By Tajirijasiri/JF
Previous
Next Post »