Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe awataka Wapanga Mipango kufanyakazi kwa Weledi, ameyasema hayo katika Mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mge. Dkt. Philip Mpango. Kaulimbiu ya Mkutano ni Kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21.
SONY DSC
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kufungua mkutano huo. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
SONY DSC
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango unaofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mge. Dkt. Philip Mpango. Kaulimbiu ya Mkutano ni Kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21.
SONY DSC
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri akizungumza katika mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango unaofanyika mjini Dodoma.
SONY DSC
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.