Staa wa muziki kutoka Afrika kusini ambaye pia ni DJ, Black Cofee ametwaa tuzo ya BET 2016 katika kipengele cha International Act Africa iliyotolewa usiku wa kumkia leo nchini Marekani.
Black Cofee amechukua tuzo hiyo na kuwashinda wasanii wenzake kama Diamond Platinumz, Wizkid, Yemi Alade, AKA, MzVee, Cassper Nyovest na Serge Beynaud.
Kwa maana hiyo mategemeo ya Tanzania na Afrika Mashariki kupata tuzo katika utoaji wa tuzo hizo kubwa duniani yamepotea baada ya mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki, Diamond Platinumz kukosa kura za kutosha kumwezesha kushinda tuzo hiyo.
Baada ya utoaji wa tuzo hizo, kinachosubiriwa kwa sasa ni utoaji wa tuzo za BET 2016 zinazowashirikisha wasanii wa Marekani ambazo zinataraji kutolewa alfajiri ya Jumatatu ya Juni, 27.