Meli ya mizigo iitwayo Happy ikitokea Dar es salaam kwenda Zanzibar imezama eneo la Chumbe, Unguja.
Taarifa
zimedai kwamba Meli hiyo ilianza kuzama saa 10 alfajiri baada ya
kuingiza maji ndani na kukosekana kwa vifaa kama motor ya kutolea maji
hayo kufikia saa 1 asubuhi hii Meli hiyo ilizama kabisa ndani ya maji.
Meli
hiyo ilikuwa imebeba Dengu gunia 450 pamoja na Mbao zaidi ya 1000 huku
wafanyakazi sita waliokuwa ndani ya Meli hiyo wakiokolewa.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ni meli ya mizigo mitupu na mabaharia mpaka sasa imeripotiwa kwamba wote ni wazima.
Sign up here with your email