Hali ya wasiwasi
iliyoanzishwa na upigaji kura wa Uingereza kuondoka Jumuiya ya Ulaya
(EU) imekumba chama kikubwa cha upinzani cha Leba.
Nusu ya Baraza
la Mawaziri la upinzani linatarajiwa kujiuzulu hii leo likilalamikia
jinsi kiongozi wao Jeremy Corbyn alivyoongoza kampeni ya kura za maoni.Wa kwanza kuondoka alikuwa Waziri wa Afya, Heidi Alexander, aliyesema kuwa Bwana Corbyn hana kipaji cha kushughulikia matatizo yanayokumba Uingereza kwa wakati huu.
Awali, Waziri wa upinzani wa Mashauri ya Kigeni, Hilary Benn, aliachishwa kazi kwa kile Bwana Corbyn alidai kuwachochea wenzake waondoke katika baraza hilo iwapo Bwana Corbyn, atakataa kuheshimu mswada wa kutokuwa na imani kwake.
Wafuasi wengi wa Leba walipiga kura kwa Uingereza kujiondoa katika Jumuiya ya Ulaya.
Sign up here with your email