Robo fainali ya pili ya michuano ya Copa America ilichukuwa nafasi usiku mwingi wa kuamkia leo huko East Rutherford, Marekani kwenye dimba la ML. Stadium ikizikutanisha Colombia na Peru.
Kabla ya mechi hii timu hizi zimewahi kukutana mara 52, Colombia akiibuka mshindi mara 20 huku Peru akipata ushindi mara 15 na wakitoka sare mara 17.
Mchezo huu ulikuwa mkali sana kwa muda wote kila timu ikitafuta nafasi za kufunga lakini walishindwa kuzitumia.
Shukrani za kipekee ziwaendee walinda milango wa timu zote mbili kwa kuokoa mipira yote ya hatari iliyoelekezwa langoni mwao. Kwa hiyo hadi mwamuzi wa mchezo huu Patricio Loustau toka Argentina anapuliza kipyenga cha mwisho dakika 90+3, Colombia 0, Peru 0.
Kulingana na kanuni za mashindano haya kutokuwa na muda wa ziada (extra time) kwa mechi za robo fainali na nusu fainali basi ikatumika kanuni ya kupigiana penati 5 kila timu, hapo ndipo Colombia walipopata penati 4 zilizowekwa kambani na James Rodriguez, Juan Cuadrado, Moreno na Perez wakati Peru walipata penati 2 zilizofungwa na Diaz na Tapia huku Trauso na Christan Cueva wakikosa. Colombia anamsubiri mshindi kati ya Mexico na Chile kwenye nusu fainali.
Wakati tukila daku usiku mwingi wa kuamkia kesho kutakuwa na hitimisho la mechi za robo fainali
ARGENTINA vs VENEZUELA na MEXICO vs CHILE
Sign up here with your email