Mataifa 6
waanzilishi wa Muungano wa Ulaya EU wanakutana leo kujadili mustakabali
wao wa baadaye baada ya Uingereza kuamua kujiondoa kutoka kwa muungano
huo.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, ufaransa,Italy,
Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi wanatarajiwa kuanzisha mchakato huo
pasi na kuwa na ngoja ngoja.Tayari rais wa tume ya muungano wa Ulaya , Jean-Claude Juncker, amesema anataka kuanzisha majadiliano mara moja ya jinsi Uingereza itakavyotoka rasmi kutoka EU .
Mawaziri hao pia wanatarajiwa kuweka masharti mapya yatakayowazuia wanachama wengine kuiga mfano wa Uingereza,baada ya vyama vya mrengo wa kulia katika mataifa mengi duniani kupongeza uamuzi huo wa Uingereza kujitoa kutoka muungano wa Ulaya...
Ameomba kuwepo kwa subra na umakini katika kulishughulikia swala hilo ambalo anasema linapaswa kuongozwa tu na vipi kushughulikia mahitaji ya raia wa jumuiya ya muungano wa Ulaya.
Sign up here with your email
