Hapa
ni ndani ya kanisa la The International Evangelical Assemblies Of God
–Tanzania (IEAGT) lililopo katika kata ya Kambarage katika manispaa ya
Shinyanga ambapo leo Jumapili Juni 26,2016 kumefanyika Maombi Maalumu
kwa ajili ya taifa la Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli,makamu wa rais,bunge,mahakama,polisi na viongozi
mbalimbali wa serikali.
Maombi
hayo yameongozwa na askofu wa kanisla la (IEAGT) David Elias Mabushi na
kuhudhuriwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Josephine
Matiro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Maombi
hayo pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali,vyama vya
siasa,mashirika,waandishi wa habari,wageni mbalimbali na waumini wa
kanisa hilo.
Pamoja
na maombi hayo maalumu, Kanisa hilo limeadhimisha siku ya watoto
katika kanisa hilo ambapo pia Juni 26 ni siku ya kuzaliwa kwa askofu wa
kanisa la IEAGT David Mabushi ambaye leo ametimiza umri wa miaka 53.
Sambamba
na matukio hayo mawili makubwa,kanisa hilo pia lilikabidhi madawati 20
kwa uongozi wa wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kumuunga mkono rais
Magufuli katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa changamoto ya madawati
inamalizika katika shule.
Awali
akisoma risala,Katibu wa kanisa la IEAGT, Mchungaji Obed Jilala alisema
baada ya uchaguzi mkuu 2015,kanisa la IEAGT limekuwa likisikia kwa
nyakati tofauti rais Magufuli akiomba maombi kwa ajili ya kazi yake ya
kuliongoza taifa,hivyo kanisa lao limeguswa sana na kauli hiyo na katika
kuonesha wanamuunga mkono walikubaliana siku ya Jumapili Juni 26,2016
iwe ya maombi maalumu kwa ajili ya kiongozi wa taifa sambamba na
kuliombea nchi ya Tanzania.
"Maombi
haya yamebebwa kwa kiasi kikubwa na upendo tulio nao kwa nchi yetu
,kanisa la IEAGT kama sehemu ya jamii ya watanzania tumeona siku ya leo
iwe kilele cha maombi ya kitaifa katika mkoa wetu na mahali popote
lilipo kanisa letu",aliongeza Mchungaji Jilala.
Naye
Askofu wa kanisa hilo David Mabushi akitoa mahubiri yake,mbali na
kumpongeza rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa rais,alimuomba kuendelea
kuonesha msimamo wake katika kuwaletea maendeleo watanzania huku
akimfananisha na Nabii Musa akisema Magufuli amekuja kuiokomboa nchi na
kuifanya kuwa nchi ya asali na maziwa.
"Tumeandaa
siku hii muhimu kwa ajili ya kuiombea nchi yetu ili iendelee kuwa na
amani,tunamuombea rais wetu kwa sababu wenye haki wakiwa na amri,watu
hufurahi..sisi kama kanisa tutahakikisha tunamuunga mkono rais Magufuli
kwa maneno na vitendo ndiyo maana leo tunatoa sadaka ya madawati
20,tunaomba watanzani waendelee kumuombea rais wetu aliyeonesha kuwajali
watanzania tangu alipoingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kupigana
dhidi ya rushwa na vitendo vyote viovu",aliongeza askofu Mabushi.
Kwa
upande wake mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Josephine
Matiro ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro,alilipongeza kanisa hilo kuona umuhimu wa kuombea viongozi wa
nchi na kuongeza kuwa kanisa la IEAGT ni kanisa la kwanza mkoani
Shinyanga kufanya maombi kwa ajili ya viongozi wa nchi.
"Ndugu
zangu watanzania naomba tuendelee kuiombea nchi ili iendelee kuwa ya
amani na viongozi kuwa na hofu ya mungu,lakini pia naomba watanzania
wafanye kazi,sasa ni muda wa kuchapa kazi tuache siasa za
majukwaani,tumuunge mkono mheshimiwa rais katika kutekeleza kauli mbiu
ya Hapa Kazi tu",aliongeza Matiro.
Miongoni
mwa mambo yaliyoombewa katika ibada hiyo ni kuombea taifa,kumuombea
rais Magufuli,makamu wa rais,waziri mkuu na viongozi wengine wa
serikali,kuombea bunge na madiwani,kuombea mahakama na katika maeneo
yote viongozi wa dini waliwataka viongozi hao kuwa hofu ya mungu na
kuchukia rushwa pamoja na kutumia nguvu zao kupambana na vitendo vya
kihalifu ikiwemo mauaji ya watu kwenye nyumba za ibada,vikongwe,albino
na watu mbalimbali wasio na hatia.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog, Kadama Malunde alikuwepo kuanzia mwanzo mpaka mwisho…ametuletea picha 74 tazama hapa chini…
Mshereheshaji
mkuu(MC) Thomas Batenga ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi
katika kanisa la IEAGT akitambulisha wageni mbalimbali kanisani
Wanakwaya
wa kwaya ya BBC ya kanisa la IEAGT wakiimba kanisani wakati wa Ibada
maalum ya maombi kwa ajili ya nchi ya Tanzania,maadhimisho ya siku ya
watoto wa kanisa hilo na zoezi la kukabidhi madawati kwa uongozi wa
serikali ya wilaya ya Shinyanga.
Meza
kuu wakiwa na mgeni rasmi,kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine
Matiro(wa pili kutoka kulia),ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya
Shinyanga.Wa kwanza ni kulia ni mwakilishi wa mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Grace Haule ambaye pia ni katibu wa UWT
wilaya ya Shinyanga vijijini,wa pili kutoka kushoto ni naibu meya wa
manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Agnes Machiya
Kushoto ni askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi akiwa na katibu mkuu wa kanisa hilo Mchungaji Obed Jilala wakiwa kanisani
Watoto
wa kanisa la IEAGT wakiimba na kucheza kanisani ikiwa leo Jumapili,Juni
26,2016 ni siku ya watoto wa kanisa hilo lililopo nyuma ya shule ya
msingi Jomu mjini Shinyanga
Watoto na waumini wengine wa kanisa hilo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani
BBC kwaya wakiimba kanisani
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani....
Askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi akizungumza kanisani
Waumini wa kanisa la IEAGT wakitafakari kanisani
Watoto wakiwa kanisani
Waumini wa kanisa hilo wakiwa kanisani
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani......
Mashemasi wa kanisa la IEAGT wakiimba kanisani
Mahubiri kwa njia ya wimbo yakiendelea
Wanakwaya wa kwaya ya BBC wakiwa wamekaa kanisani
Waandishi wa habari(mstari wa mbele) wakiwa kanisani
Watoto
wakiimba wimbo maalumu kuiombea nchi ya Tanzania na jamii kwa ujumla
huku wakihamasisha wazazi na walezi kudumisha upendo kwa watoto
Watoto wakiimba huku wamelala ..Miongoni mwa maneno yaliyokuwa yanasikika ni...."Dunia ni mbaya..changamka itakupoteza..."
Wageni waalikwa wakiwa kanisani
Katibu
mkuu wa kanisa la IEAGT ,Mchungaji Obed Jilala akisoma risala wakati wa
maombi hayo maalumu kwa ajili ya Tanzania,rais Magufuli na viongozi
mbalimbali wa serikali.Mchungaji Jilala pia ni diwani wa kata ya Lubaga
katika manispaa ya Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(
CHADEMA).
Katibu
wa kanisa hilo Mchungaji Jilala alisema baada ya uchaguzi mkuu
2015,kanisa la IEAGT limekuwa likisikia kwa nyakati tofauti rais
Magufuli akiomba maombi kwa ajili ya kazi yake ya kuliongoza taifa,hivyo
kanisa lao limeguswa sana na kauli hiyo na katika kuonesha wanamuunga
mkono walikubaliana siku ya Jumapili Juni 26,2016 iwe ya maombi maalumu
kwa ajili ya kiongozi wa taifa sambamba na kuliombea nchi ya Tanzania
Watoto wakiimba kanisani
Wazee wa kanisa la IEAGT wakiwa kanisani
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani....
BBC kwaya wakiimba wimbo maalumu wa kuiombea nchi ya Tanzania
Waumini wakiwa kanisani
Askofu
wa kanisa la The International Evangelical Assemblies of God –Tanzania
(IEAGT) David Mabushi akitoa mahubiri wakati wa ibada maalumu ya
kumuombea rais Magufuli na taifa la Tanzania.Alitumia fursa hiyo
kuwataka viongozi wa Tanzania kuwa na hofu ya mungu hali itakayosaidia
kupunguza maovu mbalimbali katika jamii
Waumini wakiwa kanisani...
Ibada inaendelea
Waumini wakimsikiliza Askofu Mabushi
Askofu Mabushi akimuombea rais Magufuli ili aongoze taifa vizuri
Askofu Mabushi akiendelea kufanya maombi kwa ajili ya rais Magufuli
Meza kuu wakimuombea rais Magufuli
Maombi yanaendelea
Waumini wakimuombea rais Magufuli na nchi ya Tanzania
Ibada ya maombi maalumu kwa ajili ya rais Magufuli inaendelea
Maombi yanaendelea....watumishi wa mungu wasoma biblia
Waumini
wakimuombea rais Magufuli ili aongoze nchi kwa hekima na busara,awe na
afya njema,asimamie kwa haki na uadilifu awe mlinzi wa nchi na kuwa
chanzo cha baraka za nchi
Askofu Mabushi na katibu wa kanisa la IEAGT Mchungaji Jilala wakiliombea taifa la Tanzania ili liwe na amani na salama
Maombi kwa ajili ya taifa la Tanzania yakiendelea
Mchungaji
Mabushi akiwa na Katibu wa kanisa la IEAGT Mchungaji Obed Jilala wakiwa
wameshikilia bendera ya Tanzania wakati wa kuliombea taifa
Waumini wakiombea nchi ya Tanzania
Maombi yanaendelea
Wazee wa kanisa wakiwa kanisani
Maombi yanaendelea
Meza kuu wakiliombea taifa la Tanzania
Maombi yanaendelea..
Mchungaji Mabushi akiendelea kuombea nchi ya Tanzania
Waumini wakitafakari wakati wa maombi hayo
Askofu Mabushi akimuombea Mgeni rasmi/Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa niaba ya viongozi wote wa nchi ya Tanzania
Askofu Mabushi akiwaombea viongozi wote Tanzania
Meza kuu wakiwa wamesimama kanisani
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani...
Mstahiki
meya wa manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni mwenyekiti wa
ALAT,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akizungumza kanisani ambapo
alilipongeza kanisa hilo kwa kufanya maombi maalumu kwa ajili ya
viongozi wa nchi
Watoto wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya kuiombea nchi ya Tanzania na viongozi wake ili watawale kwa haki
Haya
ni miongoni mwa madawati 20 yaliyotolewa na kanisa la IEAGT kama sadaka
kwa ajili ya shule zilizopo katika wilaya ya Shinyanga ikiwa ni kuunga
mkono jitihada za rais Magufuli katika kumaliza tatizo la uhaba wa
madawati katika shule
Kulia
ni Askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi akijiandaa kukabidhi
madawati kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kushoto)
Zoezi la kukabidhi madawati linaendelea
Mgeni rasmi mheshimiwa Josephine Matiro akitoa salamu za serikali wakati wa ibada hiyo
Matiro
alilipongeza kanisa hilo kwa kuandaa ibada kwa ajili ya kumuombea rais
Magufuli na kuwataka watanzania kumuunga mkono kwa vitendo badala ya
kuendesha mijadala kwenye majukwaa ya kisiasa na kuongeza kuwa hivi sasa
ni muda wa kufanya kazi tu na sio vinginevyo
Pamoja
na mambo mengine Matiro aliwataka wazazi na walezi kuwa karibu na
watoto wao kuhakikisha wanasoma na kuwaepusha dhidi ya ndoa na mimba za
utotoni
Mjumbe wa bodi wa wadhamini katika kanisa hilo Ezekiel Honga akitoa neno la shukrani baada ya ibada ya maombi kumalizika
Mgeni rasmi na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja
Mgeni rasmi,viongozi wa kanisa,wageni waalikwa na wazee wa kanisa wakiwa katika picha ya pamoja
Mgeni rasmi,viongozi wa kanisa,wageni waalikwa na mashemaji wa kanisa hilo wakiwa katika picha ya pamoja
Picha ya kumbukumbu mgeni rasmi,wageni waalikwa na viongozi wa kanisa
Mgeni rasmi na watoto
Picha zikaendelea kupigwa
Waimba kwaya ya BBC nao wakapiga picha na mgeni rasmi
Kanisa
la IEAGT lipo nyuma ya shule ya msingi Jomu mjini Shinyanga...Pichani
ni mgeni rasmi Josephine Matiro(mwenye nguo nyeusi) akiangalia choo cha
shule ya msingi Jomu kilichojengwa na kanisa hilo
Hili ni tundu la choo kati ya matundu 8 katika choo kilichojengwa na kanisa la IEAGT katika shule ya msingi Jomu
Meya
wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam(mwenye miwani),nyumba
yake ni askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi wakiwa wameongozana na
mgeni rasmi(haonekani) wakitoka kuangalia choo cha wanafunzi katika
shule ya msingi Jomu
Mgeni rasmi Josephine Matiro akitoka kuangalia choo cha wanafunzi katika shule ya msingi Jomu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka katika choo hicho
Muonekano wa choo kwa mbali (kushoto)
Mgeni rasmi Josephine Matiro akitoka katika choo hicho,akiwa ameambatana na wageni waalikwa na viongozi wa kanisa hilo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Sign up here with your email