MAAFISA BIASHARA TANGA WATAKIWA KUBADILIKA. - Rhevan Media

MAAFISA BIASHARA TANGA WATAKIWA KUBADILIKA.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella, amewataka maofisa biashara kubadilika kwa kujenga tabia na urafiki na wafanyabishara, hatua ambayo itawezesha kukusanya mapato kwa urahisi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella.
Shigella ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha uwasilishaji hoja za Mkaguzi na Mdhibti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika halmshauri ya jiji la Tanga.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema ili kuunga mkono jitihada za Rais Dk. John Magufuli katika kukusanya mapato kwa tija, maafisa hao wa TRA wanatakiwa kuepuka kutengeneza mazingira yanayofanana na uadui kwa wafanyabaishara.
Ameongeza kuwa urafiki utakaotengenezwa baina ya maafisa wa mapato utatengeneza mazingira ya wale wanaotakiwa kulipa kodi, kujihisi vyema wakati wanapotekeleza wajibu wao.
Previous
Next Post »