Siku
moja baada ya Rais John Pombe Magufuli kutangaza upya nafasi za wakuu
wapya wa wilaya nchini aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Lushoto mwenye umri
mdogo kuliko wenzake ambaye jina lake limeondolewa katika orodha hiyo
Mariam Juma,amedai kuwa nafasi aliyokuwa ameipata sio kwamba
alichaguliwa kwa upendeleo,na badala yake elimu ndio iliyosababisha
kupata hadhi ya kumuwakilisha Rais wa awamu ya nne.
Amezungumza hayo na wazazi,viongozi wa kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,pamoja na viongozi wa serikali
ngazi ya wilaya katika harambee ya kuchangia maendeleo katika chuo cha
mafunzo ya ujasiriamali kilichopo vuga wilayani Lushoto.
Awali akielezea shughuli zinazofanywa katika Chuo maalum cha
kujifunza ujasiriamali ikiwemo kutengeneza mizinga ya nyuki kwa kutumia
udongo wa mfanyanzi,elimu ya mazingira pamoja na kilimo cha mboga mboga
ili kuwapunguzia vijana changamoto za maisha,Mkuu wa chuo hicho
Mchungaji Yohana Mmaka amesema elimu ya ujasiriamali imekuwa na
mafanikio makubwa kwa kuwawezesha vijana kujitambua.
Kufuatia hatua hiyo,diwani wa kata ya Vuga wilayani Lushoto Jumaa
Dhahabu,ameiomba serikali kuu kuwahisha mafungu ya fedha za shughuli za
maendeleo katika halmashauri ya wilaya hiyo,kufuatia miradi tofauti
ikiwemo ujenzi wa maabara iliyoanzishwa na rais wa awamu ya nne
kusitishwa.
Sign up here with your email