Lile Kongamano
Kubwa la Wajasiriamali lililotarajiwa kufanyika hii leo June 11,2016
katika Uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza, limeahirishwa hadi
Julai 16,2016.
Kongamano
hilo limeahirishwa kutokana na baadhi ya washiriki kuwa katika mfungo
wa Mwezi Mtukufu na hivyo kuona si busara kufanyika.
Kongamano hilo
linatarajiwa kuwa la Kihistoria kuwahi kufanyika mkoani Mwanza kwa
kuwakutanisha Vijana Wajasirimali pamoja na Wawekezaji mkoani Mwanza
wapatao 500.
BMG inakutakia
maandalizi mema kwa ajili ya kushiriki katika Kongamano hilo ambalo
halitakuwa na kiingilio ambapo Kauli Mbiu yake inasema "Vijana Ndiyo
Mhimiri wa Upaishaji wa Pato la Taifa, Usisubiri Kesho Fursa ni Sasa".
Pichani ni Kamati
ya Maandalizi ya Kongamano Kubwa la Wajasiriamali linalofanyika hii leo
June 11,2016 katika Uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza,
ilipokutana na Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa (wa pili kushoto), wakati
ikiwa ni katika maandalizi ya kuelekea katika Kongamano hilo.
Sign up here with your email

