Shaibu Amodu
Siku chache baada ya kifo cha aliyewahi
kuwa kocha wa timu ya Taiga ya Nigeria, Stephen Keshi, kocha mwingine wa
timu hiyo maarufu kama Super Eagles, Shaibu Amodu naye amefariki dunia,
leo akiwa na umri wa miaka 58.
Amodu aliyezaliwa Aprili 1958, amefariki akiwa nchini Benini, siku tatu tu baada ya lifo cha Keshi ambaye pia alifia nchini humo.
Stephen Keshi
Wakati Keshi alidaiwa kuwa
na maumivu makali ya kichwa, Shaibu amefariki dunia baada ya kulalamika
kuwa na maumivu makali ya kifua. Inaelezwa baada ya kudai kifua kuzidi
kuuma, aliamua kwenda kupumzika na hakuamka tena. Amodu pia amewahi
kuifundisha klabu kongwe ya Afrika Kusini ya Orlando Pirates.
Sign up here with your email

