Na Mwandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko
NAAMINI kila mmoja anaufahamu
ule usemi maarufu wa bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi. Unajua kisa
chake? Kuna visa vingi vinavyounga msemo huu na miongoni ni hivi;
Mtu mmoja alikuwa ametoka katika vikao
vile vya jioni na aliporudi kwake alikuwa ameburudika kidogo, mwenyewe
akisema ni kujisahaulisha na maisha magumu aliyokuwa akiishi, hohehahe.
Kona mbili tatu, begi likawa mzigo,
lakini kuliko kuliachia kwa wenyewe, alipopita kwenye nyumba yenye
mlango wazi, akalitupia lile begi mwenyewe akiendelea na mbio kukwepa
kipigo na kifo.
Akanyata na kuufunga mlango wake, kisha
akalifuata begi lile, akalifungua. La haula, mzigo mkubwa wa hela
ulikuwa ndani yake, akapatwa na kiwewe kwa kuuaga umaskini kwa namna ya
ajabu kabisa.
Ni kwa fedha hizo, maisha yake
yakabadilika tangu siku hiyo na tunavyozungumza, alijiwekea msingi mzuri
wa familia yake ambayo hadi sasa ina maisha mazuri.
Simulizi hii ina mafunzo mengi kwako
wewe msomaji unayesoma hapa kwamba katika maisha, lolote linaweza
kutokea endapo ukimtanguliza Mungu.
Fikiria, kwa kawaida mtu yule aliyeacha
mlango wazi, alipaswa kuvamiwa, kupigwa na hata kuibiwa (ingawa alikuwa
fukara), lakini Mungu akabadili kibao na kuufanya usahaulifu wake
kumletea neema.
Hii inakufundisha kuwa mtu mwenye
kuamini katika makusudi ya Mungu. Usidharau na wala usifanye kwa kuiga,
kwa sababu mtu mwingine alipopata simulizi ile ya jamaa miaka kadhaa
mbele, naye akajenga desturi ya kuuacha mlango wake wazi, kitu
kilichomponza kwani siku moja wezi walifika na kuiba kila kilichokuwemo.
Unachotakiwa kufanya ni kutokudharau
kila unapoliona gazeti mojawapo kati ya Championi, Uwazi, Amani, Risasi,
Ijumaa na Ijumaa Wikienda. Hata kama hujanunua wewe, lakini umeliona
kipande chake kimetupwa, kiokote, kwani kinaweza kuwa na ile kuponi ya
kujishindia nyumba, itakayochezwa mwishoni mwa mwezi huu.
Ukiipata kuponi hiyo, itume kupitia
mawakala wa Global Publishers au ipeleke mwenyewe katika ofisi zao
zilizopo Bamaga Mwenge kwa wale wa Dar es Salaam.
Nakusisitiza, gazeti la leo ndilo lenye
kuponi ya ushindi, ingawa ile ya jana na juzi nazo zinaweza kutenda
maajabu. Utaichukua nyumba hii ya kisasa yenye hati, iliyojengwa eneo
tulivu na la thamani, kwa shilingi mia tano tu.
Sign up here with your email
