STORI: MWANDISHI WETU, WIKIENDA
DAR ES SALAAM:
Mwanamitindo ambaye pia ni video queen maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto, amemlipua laivu staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kisa kikidaiwa ni lile saga la kugombea penzi la kigogo (jina tunalo) ambapo kwa sasa hali ni tete baina ya wawili hao.

Hivi karibuni kuliibuka vita kali ya
matusi mitandaoni kati ya kundi la mashabiki wa Hamisa linalojiita Team
Hamisa na lile la Team Lulu ambapo kila kundi lilitaka kuibuka mshindi
huku mada kuu ikiwa ni penzi la jamaa huyo.
Wakati hali ikiwa hivyo, ilibidi wawili hao nao kuvunja ukimya na kuanza kujibizana maneno ya nguoni ambayo yalizua taharuki upya kwa kila upande.
Wakati hali ikiwa hivyo, ilibidi wawili hao nao kuvunja ukimya na kuanza kujibizana maneno ya nguoni ambayo yalizua taharuki upya kwa kila upande.
Baada ya kushuhudia malumbano hayo huku
kukiwa na maelezo kuwa wawili hao wanachonganishwa, Wikienda lilimtafuta
rafiki wa karibu wa Hamisa ili kuanika kiunaga ubaga hasira alizokuwa
nazo Hamisa ndipo aliamua kufunguka kwa kumpa makavu Lulu. Mtu huyo
alisema kuwa maneno aliyoyatumia Hamisa yalitokana na hasira na
hayaandikiki gazetini huku akifafanua kuwa yeye ana mtoto lakini Lulu
hana uchungu kwa kuwa bado hajazaa.
Baada ya kujazwa data hizo, Wikienda
lilianza kwa kumtafuta Hamisa ili kupata ufafanuzi juu ya sakata hilo
ambapo alisema kuwa utaratibu aliojipangia kwenye maisha yake ya siku
hizi ni kutotoa taarifa zake kwa waandishi wa habari hivyo asingependa
‘ku-coment’ lolote juu ya hilo japokuwa kila suala lipo wazi.
“Kusema kweli maisha ya sasa kuna muda
unaweza kujikuta ukiingizwa kwenye ugomvi ambao hukutarajia na hivyo kwa
kuzingatia hilo nisingependa kuongelea tena habari hii maana utaratibu
wangu ni kutotoa taarifa wala mambo yangu kuyaweka wazi kwenye magazeti
ila kilichoonekana ndicho hicho kwa sasa sina coment yoyote,” alisema
Hamisa.
Kwa upande wake Lulu alijibu mapigo kwa
kuandika waraka mrefu bila kumtaja Hamisa lakini wapenda ubuyu
wakatafsiri kuwa ujumbe umefika. Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mgogoro
kati ya Hamisa na Lulu huku madai ya msingi yakiwa ni kitendo cha Lulu
kumchukulia Hamisa baba mtoto wake.
Sign up here with your email