WANANCHI WA KITONGOJI CHA PERA CHALINZE WAANZA KAMPENI YA KUPAMBANA NA MLIPUKO WA KIPINDUPINDU. - Rhevan Media

WANANCHI WA KITONGOJI CHA PERA CHALINZE WAANZA KAMPENI YA KUPAMBANA NA MLIPUKO WA KIPINDUPINDU.

Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze Hussein Mramba akizungumza na wafanyabiashara mbali mbali wa kitongoji cha Pera Chalinze katika mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kujadili namna ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa kipindu pindu.
 Baadhi ya wafanyabishara katika kitongoji cha pera Chalinze wakiwa katika Mkutano huo wa kujadili masuala ya usafi pamoja na kupambana na kipindupindu. 

KATIKA kuunga  mkono juhudi za serikali katika kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu  wafanyabiashara  mbali mbali katika kitongoji cha Pera halmashauri ya Chalinze  Mkoa wa Pwani  wameungana na kuanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kutokomeza  taka zote  zinakuwa zikitupwa ovyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  katika kikao  kilichoandaliwa kwa ajili ya kuweza kujadili  mambo mbali mbali  kuhusiana na suala la usafi pamoja na kupanga mikakati ya kuweza kuhakikisha wanapambana  vilivyo na mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu.


Previous
Next Post »