Mara baada ya tmu ya Simba SC kupoteza mchezo wa jana kwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mashabiki wameutaka uongozi uliopo hivi sasa kujiuzulu na kuacha timu kwa uongozi mwingine.
Wakizungumza leo Jijini Dar es Salaam mashabiki hao wamesema, viongozi hawawajali wacherzaji wala mashabiki hivyo wanachangia kwa asilimia kubwa timu kufanya vibaya katika hatua ya lala salama kunako michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Mashabiki hao wamesema, hawakubaliani na uongozi uliopo hivi sasa kwani imefikia hatua kuitwa majina ya ajabu kutokana na timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika mechi za Ligi Kuu.
Mashabiki hao wamesema, viongozi waliopo wanaonyesha hawana uchungu na timu hasa pale inapofanya vibaya hivyo ni bora wawaachie wenye uchungu na timu na watakaoweza kuleta maendeleo katika klabu hiyo.
Simba SC imekuwa ikipata matokeo mabaya katika michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara katika hatua hii ya lala salama ambapo katika mchezo dhidi ya Toto African ya jijini Mwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Aprili 17 mwaka huu Simba pia ilipoteza kwa bao 1-0 suala lililopelekea baadhi ya wachezaji ya Simba kuhusishwa katika kuhujumu timu.
Sign up here with your email