Mamlaka ya Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi wa sukari tani 6757 mali ya Kampuni ya El-Naeem Enterprises iliyokamatwa hivi karibuni katika Bohari ya Forodha ambapo imesema ilikuwa chini ya uangalizi ikisubiri vibali husika ili iweze kuruhusiwa kusambazwa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Richard Kayombo, amesema sukari hiyo ilikuwa katika Bohari ya Forodha ya uangalizi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwa imehifadhiwa kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kodi, vibali vya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na vibali vya Bodi ya Sukari na hatimaye kuweza kuruhusiwa kutoka.
Sukari hiyo kwa sasa imeruhusiwa kutolewa ambapo mtembezi.com imefika katika bohari hiyo na kushuhudia ikipakuliwa tayari kusambazwa nchini.
Sign up here with your email