Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Boniface Jacob akiongea na waandishi wa habari
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Boniface Jacob ametangaza kumsimamsha kazi mwanasheria mkuu wa manispaa hiyo, Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Einhard Chidaga.
Uamuzi huo umechukuliwa kwa kauli moja na madiwani wa manispaa hiyo kufuatia kikao chao mwishoni mwa mwezi uliopita.
Mheshimiwa Jacob amewaeleza waandishi wa habari kuwa wawili hao wameisababishia hasara kubwa, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.
Makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo ni:
1. Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa
Manispaa vilipaswa kupata shilingi milioni 900 kwa mwaka kwa uwekezaji huo. Lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba mapato hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi bilioni 4.5 mpaka sasa.
2. Mgogoro wa wapangaji wa nyumba za Magomeni Kota
Manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota, hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa nyumba hizo longer, wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika nyumba na kutoa madai ya kujengewa nyumba ama kulipwa fedha za fidia kutokana na Usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama imeruhusu iliamuru Manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji nje ya mahakama.
Sign up here with your email