Korea Kaskazini imesema kuwa itatumia silaha zake za nyukilia kujilinda rais Kim Jong-unamesema.
Kiongozi wa wa taifa hilo lenye usiri mkubwa Kim Jong-un aliwaelezea wajumbe wa kamati kuu ya chama tawala Workers' Party mjini Pyongyang kuwa jeshi lao litatumia silaha hizo za kitonoradi kulinda uhuru wa taifa hilo utakapotishiwa.
Aidha rais Kim jong un aliwaeleza wajumbe hao kuwa Korea Kaskazini sasa itaanza kusemezana na mataifa yaliyokuwa mahasidi wao hapo awali.
Vyombo vya habari vya taifa vimemnukuu kiongozi huyo akiambia baraza Kuu la chama cha wafanyikazi kinachotawala kuwa kunapaswa kuwepo mashauriano zaidi na Korea Kusini ili kuimarisha uelewano na kuaminiana.
Inadaiwa pia kuwa alisema kuwa serikali yake itafanya kila juhudi kupunguza kuenea kwa silaha za kinyukilia duniani ingawa taifa lake lilijiondoa katika chama cha kupunguza ongezeko la zana za kinukilia duniani mwaka 2003.
Korea Kaskazini ilifanya jaribio la silaha yake ya kinukilia miaka mitatu baadaye na kuna uvumi kuwa inatarajia kufanya jaribio la tano ili kwenda sambamba na mkutano wa baraza Kuu la Cchama tawala unaondelea hivi sasa.
Mara kadhaa serikali ya Korea Kaskazini imetisha kushambulia Marekani na Korea Kusini kwa mabomu ya kinyukilia.
Sign up here with your email