Mwandishi wa habari ambaye pia ni mkereketwa wa haki za kibinadamu, Khurram Zaki, amepigwa risasi na kuuawa jijini Karachi, Pakistan.
Ripoti zinasema kuwa alikuwa akila chakula katika mgahawa mmoja wakati alipopigwa risasi na washukiwa wanne waliokuwa kwenye pikipiki.
Watu wengine wawili walijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.
Khuram Zaki alikuwa mhariri wa gazeti moja kwenye mtandao lijulikanalo kama "Tujenga Pakistan , ambalo linashutumu mgawanyiko na kuitisha ustawi wa demokrasia na maswala yasiyoandamana na dini.
Ukereketwa wake wa hivi majuzi ni kuwashutumu wale waliochochea chuki na uhasama dhidi ya Waislamu Washia.
Majuzi tu alikashifu udhalilishwaji wa imamu wa msikiti mwekundu ulioko Islamabad.
Bw Zaki na wengine walikwenda mahakamani kumshtaki bwana Abdul Aziz kwa kuchochea uhasama dhidi ya waislamu wachache wa kishia.
Madai hayo yanatokana na kauli ya kadhi huyo kukataa katakata kukashifu shambulizi la kigaidi katika shule moja mjini Peshawar mwaka wa 2014 ambapo wanafunzi 152 waliuawa.
Sign up here with your email