Kamati
Kuu ya Chadema itakutana mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba
kuanzia Mei 11 Jumatano na Alhamisi kitakachojadili mwenendo wa Serikali
ya CCM chini ya Rais John Magufuli.
Taarifa
iliyotolewa leo na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini
Makene imesema kikao hicho, pamoja na mambo mengine, kitajadili taarifa
ya hali ya siasa nchini.
Pia
kikao hicho kitajadili na kupitisha mpango kazi wa chama kwa mwaka huu
unatokana na Mpango Mkakati wa Chama wa miaka 5 kabla ya Sekretarieti
kuanza utekelezaji.
Mpango
huo utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na
uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi.
Sign up here with your email