WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA DK HARRISON MWAKYEMBE AMEAPA KUFA NA KUPONA KWA WAUAJI WA WALEMAVU WA NGOZI - Rhevan Media

WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA DK HARRISON MWAKYEMBE AMEAPA KUFA NA KUPONA KWA WAUAJI WA WALEMAVU WA NGOZI



Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Harrison Mwakyembe (pichani) ameapa kuwa wizara yake kwa kushirikiana na ile ya Mambo ya Ndani ya Nchi itapambana kufa au kupona na watu wanaoua wenye ulemavu wa ngozi nchini hususan kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.Dk Mwakyembe aliyasema hayo jijini Mwanza wakati alipozungumza na watendaji na wafanyakazi walio chini ya wizara yake jana mkoani hapa.“Tumefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kuona ni namna gani tutaunganisha nguvu pamoja ili tuweze kukabiliana na changamoto zilizo kwenye wizara zetu,” alisema.
Dk Mwakyembe alisema wizara hiyo inakerwa na mauaji ya albino ambayo alisema Mkoa wa Mwanza ndio unaongoza kwa mauaji hayo.“Mkoa wa Mwanza unaongoza kwa mauaji ya albino ukifuatiwa na mkoa wa Kagera, kwa mauaji haya tumedhalilika kama taifa. Ilifikia wakati hata ukienda nje ya nchi unaogopa kugawa ‘business card’ yako kwa kuogopa kusemwa na watu juu ya suala la mauaji ya albino,” alieleza.
Previous
Next Post »