MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) IMETOA TAHADHARI KWA WAKAZI WA MIKOA ZAIDI YA TANO. - Rhevan Media

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) IMETOA TAHADHARI KWA WAKAZI WA MIKOA ZAIDI YA TANO.



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari kwa wakazi wa Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja, kwamba kutakuwapo na mvua kubwa kuanzia Aprili 13 hadi 16, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mvua hizo zitanyesha kwa mfululizo zitakazozidi milimita 50 ndani ya saa 24 zikiwa ni za wastani wa asilimia 70.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua sambamba na uwapo wa kimbunga kiitwacho `Fantala' katika Bahari ya Hindi.TMA imewataka wakazi wa mikoa hiyo iliyotajwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki.
Aidha, imesema TMA inaendelea kufuatilia hali hiyo na itakuwa inatoa mrejesho kila wakati.
Previous
Next Post »