WATUHUMIWA WA KESI YA TUMBILI WASOTA MAHAKAMANI. - Rhevan Media

WATUHUMIWA WA KESI YA TUMBILI WASOTA MAHAKAMANI.



Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

HATMA ya dhamana kwa washtakiwa saba wa makosa ya uhujumu uchumi wakiwamo wafanyabiashara raia wa Uholanzi waliokamatwa Machi 23 mwaka huu wakijaribu kusafirisha wanyama hai 61 aina ya Tumbili sasa kujulikana Alhamisi (Aprili 14).

Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji wa mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi ,Aishiel Sumari wakati akitoa uamuzi mdogo juu ya hoja zilizotolewa na upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Majura Magafu dhidi ya upande wa Jamhuri kuhusu maombi ya dhamana kwa washtakiwa.
 
Hoja za upande wa utetezi zilitokana na upande wa Jamhuri kuwasilisha mahakamani hapo hati zuio la dhamana kwa washtakiwa wote saba iliyotoka kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Maombi matatu ya dhamana yaliwasilishwa mahakamani hapo ambayo ni ombi la tatu la raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian ,Eduard Vardanyan na Idd Misanya ,ombi nne la ,Nyangabo Musika,Martina Nyakanga na Very Anthon huku ombi la tano lilikuwa ni la aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa idara ya wanyamapori nchini Dkt Charles Mulokozi.

Baada ya maombi hayo kuwasilishwa upande wa utetezi uliridhia kuunganishwa kwa maombi hayo ili kuokoa muda wa mahakama katika kusikiliza shauri hilo baada ya maombi hayo kufanana.Akitoa uamuzi huo Jaji Sumari aliuelekeza upande wa jamhuri kupitia kwa wanasheria wa Serikali Wankyo Simon na Robart Rogart kutumia siku ya leo (Jumanne) kuwasilisha hoja kinzani na kwamba upande wa utetezi utawasilisha maombi yao kesho (Jumatano) baada ya kujibiwa na upande wa pili.
Baadhi ya Washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi ya usafirishaji wa wanyama Hai 61 aina ya Tumbili wakiongozwa na asakari Polisi walipokuwa wakiwasili katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi.
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakisindikizwa na askari Polisi kuingia mahakamani,Nyuma yao ni mshtakiwa mwingine Idd Misanya . Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi ,kulia ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt Charles Mulokozi. 



Previous
Next Post »