Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bwana Richard Kasesela leo (jana) amefungua Warsha ya
mwanzo wa mradi wa utafiti wa "HALI YA MAJI CHINI YA ARDHI KATIKA
AFRIKA, KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA" katika hotel ya Gentle Hill. Mradi
huu unafanywa na chuo kikuu SUA na Gro `Futures.
Akizungumza katika hotuba yake alisema;Matumizi
ya maji chini ya ardhi yamekua kwa kasi zaidi hivi karibuni kutokana na
maendeleo ya maarifa ya elimu ya sayansi. Changamoto kubwa ni udhibiti
wa rasilimali hii chini ya ardhi haujaenda sambamba na ongezeko hili la
mtaumizi. Hivyo basi utafiti huu utasaidia kutengeneza utaratibu
thabiti wa matumizi ya maji yaliyo chini ya ardhi.
Uchumi
wa nchi ya Tanzania kiasi kikubwa unategemea uwepo wa maji, utunzaji
na mipango thabiti itasaidia Tanzania kusonga mbele. Umefika wakati sasa
kwa nguvu zote tusimamie maji tuliyo nayo kwa kuwa na mkakati wa pamoja
wa maji yaliyo juu ya ardhi na yale ya ardhini.
Nampongeza
sana Prof Japhet Kashaigili ambaye ndie mtafiti Mkuu pamoja na Prof
Richard Taylor Mtafiti mwandamizi kwa kuchagua Iringa kuwa kituo cha
utafiti naamini mkoa utanufaika si tu na matokeo ya utafiti bali pia
baadhi ya wana sayansi wetu kushiriki kwenye utafiti."
Wadau wa Warsha hiyo wakimsikiliza Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bwana Richard Kasesela (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza

Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bwana Richard Kasesela pichani kati akiwa na Prof Japhet Kashaigili ambaye ndie mtafiti Mkuu pamoja na Prof
Richard Taylor Mtafiti mwandamizi
wakiwa katika picha ya pamoja na Wadau wengine wa Warsha hiyo
Sign up here with your email