Wanawake zaidi ya 500 wa kijiji cha Nakwa katika halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara wamelazimika kuaandamano na kuvamia ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kutafuta suluhu ya kuepukana na vitendo vya unyanyasaji, ubakaji, ulevi uliokithiri kwa wanaume na kunyimwa haki zao za ndoa na kuepuka vitisho vya kuuwawa na wafanyabiashara wa pombe haramu ya Moshi na wanywaji wao endapo watawafichua.
Wakizungumza na ITV wakiwa katika maandamano hayo waliotembea umbali wa km saba huku wakiwa na mabango yenye kupinga unyanyasaji huo hadi kuifika ofisi hiyo ya mkuu wa wilaya, wamesema tayari kutokana na vitendo hivyo ambavyo vimesababisha mauaji ya wanawake, na sasa wanalazimika kupeleka malalamiko hayo baada ya serikali ya kijiji hicho kuonekana kushindwa kuthubutu kuchukua hatua, wakiwa mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya wimbo ni kudai haki.
Nae mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho cha Nakwa Bw Steven Qwatlema amekiri kukithiti kwa biashara hiyo ya pombe haramu ya Moshi inayotengenezwa pembezoni mwa ziwa Babati na kukiri kushindwa kuchukua hatua kutokana na uzito wa hali halisi.
Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya Babati Bw Crispin Meela akiwataka polisi kuanza kuendesha msako wa nyumba kwa nyumba wa kukamata makundi ya wafanyabiashara, wakiwemo wafanyabiashara wa Pooltable na kuwataka kutoa taarifa za ubakaji ndani ya saa 72.
Sign up here with your email