WANAKIJIJI WAMTUMBUA MWENYEKITI WILAYANI HAI. - Rhevan Media

WANAKIJIJI WAMTUMBUA MWENYEKITI WILAYANI HAI.


Wananchi wa Kijiji cha Shirinjoro Kata ya Mnadani Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wamemng'oa Madarakani Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho Clemence Nkya kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji wa Chanzo cha Maji pamoja na kuingia mikataba mbalimbali bila kuwashirikisha wananchi wa Kijiji hicho.
Duru Kijijini hapo zinaeleza kuwa Mwenyekiti huyo pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kitifukati wamekuwa wakijichukulia Mamlaka wao wenyewe pasipo kutoa taarifa yoyote kwa wananchi.
Previous
Next Post »