MKUU WA MKOA MWANZA ACHARUKA VIBAYA. - Rhevan Media

MKUU WA MKOA MWANZA ACHARUKA VIBAYA.





Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha linakabidhi kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la Bugando ifikapo Aprili 25, 2016 kwa mmiliki halali wa kiwanja hicho bwana Justine Eminoga ambacho amekuwa akikidai kutoka kwa mfanyabiashara wa Jijini humo kwa zaidi ya miaka sita sasa.

Mongella amefikia hatua hiyo mara baada yakupokea malalamiko kutoka kwa bwana Justine ambaye alifika katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala lake ambalo limedumu kwa zaidi ya miaka sita sasa. Akitoa malalamiko yake mbele ya mkuu huyo wa mkoa, bwana Justine alidai kuzulumiwa kiwanja hicho na mfanyabiashara aliye mtaja kwa jina Shanif Mansour ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwimba.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuhakiki watumishi, ili kubaini endapo kuna watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali, zoezi la sasa ambalo linasimamiwa na Ofisi ya katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa kamati maalumu zilizo undwa na mkuu wa Mkoa huo, 

Akiwa katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa aliagiza kukamatwa kwa Afisa Utumishi msaidizi wa jiji la Mwanza Henry Sedetale, ambaye alisaidia watumishi hewa watano kuchukua mikopo ya zaidi ya Mil.90 kutoka katika benki tofauti tofauti, hata hivyo taarifa kutoka Taasisi yakupambana na kuzuia rushwa mkoani Mwanza iliyotolewa wakati wa kikao hicho na mkuu wa Takukuru mkoani humo, ilisema mtuhumiwa huyo tayari alikuwa ametiwa nguvuni na taasisi hiyo kwa mahojiano zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza yupo katika ziara kujitambulisha katika mkoa huo na hii ikiwa ni Wilaya yake ya tatu mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi na Magu hapo awali.

Imetolewa na
Atley J. Kuni
AFISA HABARI NA MAHUSIANO –RS MWANZA. 18 Aprili, 2016

Previous
Next Post »