WAKUU WA IDARA TANO WAANZA KUCHUNGUZWA . - Rhevan Media

WAKUU WA IDARA TANO WAANZA KUCHUNGUZWA .


Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani limeunda kamati itakayochunguza tuhuma zinazowakabili wakuu wa idara tano waliohusika katika kuvurunda na kushindwa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya umwagiliaji,ardhi na ujenzi ili kuwachukulia hatua zinazostahiki.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya baraza hilo kujigeuza kamati ili kuwajadili wakuu wa idara walioguswa katika tuhuma hizo ambapo Mwenyekiti wa Halmashsuair hiyo Bw.Juma Abeid mara baada ya kikao hicho akatoa maamuzi waliyokubaliana katika kikao chao.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Bi.Martha Mkupasi amesema kikao hicho kilikuwa cha kawaida kilicholenga kupokea taarifa za utendaji kazi za kawaida za robo Mwaka katika idara husika kuanzia Mwezi Oktoba hadi Desemba Mwaka jana na kukiri kuwa kikubwa kilichojitokeza ni uzembe kwa baadhi ya wakuu wa idara katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya Maendeleo ya wananchi.
Previous
Next Post »