WAHAMIAJI 400 WAHOFIWA KUZAMA BAHARINI. - Rhevan Media

WAHAMIAJI 400 WAHOFIWA KUZAMA BAHARINI.



wahamiajiImage copyrightLibyan Coastguard
Image captionMaelfu ya wahamiaji kutoka Afrika na Mashariki ya Kati wamekuwa wakijaribu kufika Ulaya
Wahamiaji karibu 400, wengi wao kutoka Somalia, wanahofiwa kuzama katika bahari ya Mediterranean wakijaribu kuelekea bara Ulaya.
Taarifa kutoka Misri zinasema wahamiaji hao walikuwa wakitumia boti nne kusafiri.
Jamaa za baadhi ya wahamiaji hao wamesema baadhi ya wahamiaji waliokolewa na kikosi cha wana maji kutoka Ugiriki na sasa wamo Ugiriki.
Balozi wa Somalia nchini Misri amethibitisha kisa hicho lakini akasema bado wanatafuta maelezo zaidi.
Previous
Next Post »