
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo atawasha Mwenge wa Uhuru na kuzindua rasmi mbio zake ili kukimbizwa katika halmashauri za wilaya na Manispaa zipatazo 179 za mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.Uzinduzi huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambao utatanguliwa na shamrashamra za halaiki kutoka kwa vijana zaidi ya 1,000 na vikundi vya utamaduni kutoka wilaya za Morogoro na nje ya mkoa huo.Katika uzinduzi huo, viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na vyama vya siasa wamealikwa kushiriki wakiwemo pia mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Miongoni mwa mawaziri ambao hadi jana walikuwa tayari wamewasili mkoani hapa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Sera, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mouldine Castico.
Sign up here with your email
