
Raia wawili wa China wamehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela au kulipa faini ya Sh milioni 50 kila mmoja, kwa kosa la kusafirisha Sh milioni 20 kwenda nchini China bila kibali kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha baada ya washtakiwa kukiri kosa. Washtakiwa waliohukumiwa kifungo hicho ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Feng Shi Trading, Sun Ning (39) na Fen Quan (51).Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema washitakiwa wamepatikana na hati ya makosa matatu, na kwa kosa la kwanza kila mmoja atalipa faini ya Sh milioni 10 au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela, kosa la pili faini ya Sh milioni 20 au jela miaka mitano, kosa la tatu faini ya Sh milioni 20 au jela mwaka mmoja.
Alisema kwa makosa yote, adhabu yao ni sawa na kifungo cha miaka 11 jela au kila mmoja kulipa faini ya Sh milioni 50, lakini adhabu ya kifungo inakwenda sambamba hivyo ni sawa na kifungo cha miaka mitano jela
Sign up here with your email