Wabunge nchini Afrika kusini watawasilisha hoja ya kumshitaki rais Jacob Zuma baadaye leo ikiwa ni baada ya mahakama kuu ya nchi hiyo kutoa hukumu kwamba rais huyo alikiuka katiba kwa kutumia mamilioni ya dola fedha za umma kukarabati nyumba yake ya binafsi.
Chama kikuu cha upinzani, The Democratic Alliance, kilitoa wito wa Zuma ashitakiwe baada ya mahakama ya katiba kutoa hukumu wiki iliyopita.
Lakini Zuma huenda akanusurika na changamoto hiyo, wakati bunge la nchi hiyo litahitaji wingi wa theluthi mbili kuweza kumshitaki wakati chama tawala cha African National Congress , ANC , ambacho kinamuunga mkono Zuma ambaye ni rais wa chama hicho pia, kina wingi wa kutosha bungeni hivyo kumuwezesha kukwepa kihunzi hicho.Sign up here with your email