UJENZI WA SHUKE YA KUMBUKUMBU YA SOKOINE WAKWAMA. - Rhevan Media

UJENZI WA SHUKE YA KUMBUKUMBU YA SOKOINE WAKWAMA.


Juhudi za Ujenzi za ujenzi wa shule ya kumbukumbu ya Sokoine katika eneo alilopata ajali Hayati Moringe Sokoine, la Wami Dakawa Sokoine, zimezidi kufifia kutokana na kutokamilika kwa Ujenzi wa Shule hiyo.
Eneo la Wami Dakawa alipopata ajali Hayati Edward Moringe Sokoine ambapo inatakiwa kujengwa shule ya Sokoine Memorial
Shule hiyo ambayo ujenzi wake ulinza tangu mwaka 2009 bado haujakamilika hadi leo zaidi ya jengo la utawala hali ambayo inafifisha jitihada za kutunza kumbukumbu ya Hayati Edward Moringe Sokoine.
Akizungumzia sababu za kushindwa kuendelea kwa Ujenzi wa Shule hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bi. Elizabeth Mkwasa amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo umekua ukisuasua kutokana na rasimali pesa kutoka serikalini.
Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro Elia Mtandu, amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo ya Sokoine Memorial ulibuniwa na mkoa mwaka 2009 lakini umeshindwa kuendelea kwa kasi kutokana na ukosefu wa fungu la fedha lakini wapo katika mchakato wa kuikamilisha.
Nao Wakazi wa Wami Dakawa Sokoine nao wameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ili kutunza kumbukumbu ya kiongozi huyo ambae ni wa kupigiwa mfano nchini.
Jana ilifanyika ibada ya kumbumbuku ya miaka 32 ya kifo cha Edward Moringe Sokoine ambayo ilihudhiriwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli na pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya dini.
Previous
Next Post »