TAKUKURU WAMCHARUKIA MKURUGENZI WA TANESCO. - Rhevan Media

TAKUKURU WAMCHARUKIA MKURUGENZI WA TANESCO.



Kufuatia wadau wengi kuhitaji kujua hatua zitakazochukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) dhidi ya hukumu ya kesi ya rushwa Na. 75/2014 iliyokuwa ikimkabili Bw. William Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wenzake watano.

TAKUKURU inapenda kuufahamisha umma kwamba inafanya taratibu za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa tarehe 14/4/2016 na Mhe. Hakimu Mkazi Hellen katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaniaba ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Kyey Rusema. Katika hukumu hiyo washtakiwa wote sita (6) waliachiwa huru.

Aidha, TAKUKURU inawataka wadau na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba ni utaratibu wa kisheria kwamba upande usioridhika na hukumu iliyotolewa kukata rufaa katika Mahakama ya juu.


Previous
Next Post »