JIJI LA TANGA LAPATA UGENI MZITO. - Rhevan Media

JIJI LA TANGA LAPATA UGENI MZITO.



                Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara za Vetenari Tanzania "TVLA" Dkt. Furaha Mramba akiwakaribisha baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Oman waliopo nchini kwa ziara ya siku tatu (3) inayomalizika leo, ambao walitembelea katika Taasisi  ya utafiti na uchunguzi wa wadudu na magonjwa waenezayo "VVBDRI -TANGA" inayosimamiwa na wakala hiyo na kutembelea sekta ya mifugo ili kuweza kujionea fursa za uwekezaji kupitia miradi hiyo.
 Kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Oman Bw. Warith Al- Kharusi akieleza  malengo ya ziara yao Mkoani Tanga ambapo alieleza kuwa wamekuja kutembelea mradi wa shamba la mifugo ili waweze kujionea fursa za uwekezaji zinazoweza kupatikana kupitia mradi huo na miradi mingine watakayoitembelea.  
 Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Omani wakiongozwa na viongozi wakuu na maafisa  wa Taasisi za TVLA na VVBDRI-TANGA wakiwasili katika shamba la utafiti Mivumoni lililopo Wilayani Pangani Mkoani Tanga lenye ukubwa wa ekari 12789.6 ili kuweza kuona shughuli za ufugaji zinazofanyika katika shamba hilo

 Bw. Warith Al - Kharusi akijadili jambo na wafanyabiashara wenzie wakati walipokuwa wakitembelea shamba hilo linalofuga Ngo'mbe, mbuzi na Kondoo, ambapo mpaka sasa Taasisi ya VVBDRI - Tanga imeweza kutumia asilimia 20 ya shamba hilo kwaajili ya shughuli za ufugaji na sehemu inayobaki bado haitumiki.



Previous
Next Post »