SERIKALI YAITAJIKA KUKABIDHI KINU CHA USAGISHAJI. - Rhevan Media

SERIKALI YAITAJIKA KUKABIDHI KINU CHA USAGISHAJI.

Kamati ya kudumu ya Bunge,Kilimo Mifugo na Maji, imesisitiza serikali kuharakisha mchakato wa kukabidhi kinu cha usagishaji kilichopo Arusha kwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ili ianze uzalishaji mara moja.




Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Kilimo Mfugo na Maji, Dkt. Christine Ishengoma.


Akiongea mara baada ya kutembelea kinu cha Nafaka mchanganyiko Mkoani Iringa ambacho kimeanza kazi Mwaka jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Christine Ishengoma amesema hatua hiyo itasaidia wananchi kuepukana na baa la Njaa.
Dkt. Ishengoma amesema kuwa kamati hiyo imeridhishwa na utendaji kazi wa Kinu cha Iringa hivyo wameitaka serikali kutatua mgogoro wa kimktaba ili wakabidhi kinu cha mazao mchanganyiko cha mkoani Arusha.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe William Ole Nasha amesema serikali inathamini mchango wa vinu vya taifa katika uhifadhi wa chakuka utakaosaidia wakati wa maafa.
Ole Nasha amesema kuwa kutokuwa na Msagishaji wa Umma inawezea kuleta changamoto kwenye usalama wa Chakula kwa sababu wasagishaji binafsi huagalia zaidi biashara yao hivyo lazima serikali iwe na vinu vyake katika uhifadhi wa Chakula.
Previous
Next Post »