KAMATI YANUSA UFISADI JENGO LA MAKAMU WA RAIS. - Rhevan Media

KAMATI YANUSA UFISADI JENGO LA MAKAMU WA RAIS.

Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imeagiza kufanyika uchunguzi wa matumizi ya zaidi ya Shilingi bilioni 8 za ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya makamu wa rais na kusimamishwa kwa ujenzi wake kutokana na kubainika kasoro nyingi katika jengo hilo.




Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na sheria wakisikiliza kwa makini taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mohammed Mchengelwa amesema hayo wakati akitoa majumuisho baada ya kuhitimisha ziara ya ukaguzi wa miradi ya serikali zilizofanywa na kamati hiyo kwa muda wa wiki moja.
Kwa mujibu wa Mchengelwa licha ya jengo hilo lililopo mtaa wa Albert Luthuri Jijini Dar es Salaam, kuwa na mapungufu mengi na nyufa tayari asilimia 98 ya malipo ya jengo hilo yamefanyika ambapo katia ya shilingi bilioni 8 ni shilingi milioni 240 ndio zimebaki kabla ya kukabidhiwa kwa mradi huo.
Kamati pia imetaka ripoti kutoka kampuni ya Ujenzi wa Mecco na wakala wa Ujenzi TBA,ili kujiridhisha na uhalisia wa malipo ya Ujenzi kulingana na kiwango cha jengo hilo kabla halijaaanza kutumika.
Jengo hilo jipya linatarajiwa kuwa ofisi mpya ya Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Previous
Next Post »