SELIKALI YATAKIWA KUKUMBUKA MAHABUSU YA WATOTO. - Rhevan Media

SELIKALI YATAKIWA KUKUMBUKA MAHABUSU YA WATOTO.


Serekali imetakiwa kuangalia kwa makini mahabusu ya watoto ya mkoa wa Arusha kwani mahabusu hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa majengo pamoja na ukosefu wa dawa na usafiri kwa ajili ya mahabusu hiyo.Hayo yameelezwa juzi na baadhi ya wajumbe wakamati ya utekelezaji Jumuia ya wazazi wilaya ya Arusha wakati walipotembelea na kutoa msaada katika mahabusu hiyo ya watoto ilipo ndani ya jiji la arusha .

Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya wazazi ccm wilaya Arusha Rehema mohamed aliitaka serekali kuangalia kwa makini sana mahabusu hiyo kwani watoto wanaoishi katika mahabusu hiyo wamekuwa wanateseka sana kutokana na mazingira ya mahabusu hiyo.Aidha aliitaka pia mahakama kujitaidi kusikiliza kesi za watoto hao kwani wengi wao wamekaa kwa kipindi cha mda mrefu bila kesi zao kusikilizwa na badala yake wamekuwa wakiambiwa kila siku upelelezi auja kamilika.

katibu wa Jumuiya ya wazazi ccm wilaya Arusha Rehema mohamed katikati akiwa na wajumbe wengine wa Kamati ya utekelezaji Jumuia ya wazazi wilaya ya Arusha wakati walipotembelea mahabusu ya watoto iliopo ndani ya jiji la Arusha hii ikiwa ni moja ya sehemu yao ya kuazimisha sherehe ya wiki ya wazazi Tanzania
wajumbe wakewa wanasubiri kukabidhi baadhi ya vifaa ambavyo walienda kukabidhi katika mahabusu hiyo ya watoto
wajumbe wakiwa wanamkabidhi Afisa ustawi wa jamii wa mahabusu ya watoto Arusha baadhi ya vitu ambavyo walivipeleka kwa ajili ya watoto hao
mmoja wa wajumbe ambaye jina lake alikuweza kufahamika mara moja akiwa anatandika kitanda mara baada ya kupeleka vitu mbalimbali ikiwemo shuka hizo.

Previous
Next Post »