SABABU YA SIMBA KUMTIMUA HASSAN KESSY . - Rhevan Media

SABABU YA SIMBA KUMTIMUA HASSAN KESSY .


Klabu ya soka ya Simba imemsimamisha mchezaji wao Hassan Kessy Ramadhan mechi tano kwa kosa la kumchezea madhambi mshambuliaji wa Toto Africans Edward Christopher. Katika Mchezo uliochezwa April 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa Kessy alimchezea Christopher faulo, hivyo kupewa kadi nyekundu, na uongozi Simba umeamua kumfungia mechi hizo ili kupinga Vitendo vya Utovu wa nidhamu.


Kufungiwa mechi tano kwa Kessy maana yake ni kuwa amefungiwa hadi Mwisho wa msimu kwani Simba imebakisha mechi tano katika msimu huu. Hii inamaanisha kuwa Hassan Kessy Ramadhan si mchezaji tena wa Simba maana mechi tano alizosimamishwa ni sawa na mwezi mmoja ambao ni muda wa mkataba wake uliosalia.
Previous
Next Post »