PICHA 11: WALIO FARIKI BAADA YA AJILI YA GARI KUZAMA BAHARINI LEO. - Rhevan Media

PICHA 11: WALIO FARIKI BAADA YA AJILI YA GARI KUZAMA BAHARINI LEO.

Kigamboni (1)Zoezi la uokoaji likiendelea ndani ya Bahari ya Hindi.Kigamboni (2)Mwili wa marehemu Nice Mwakalago baada ya kupatikana.Kigamboni (4) 
Mwili wa marehemu ukishushwa nchi kavu baada ya kuokolewa.Kigamboni (5)Kigamboni (6)
Mwili wa marehemu ukipelekwa kwenye gari la polisi ili ukahifadhiwe hospitali.Kigamboni (9) 
Mwili wa marehemu ukipakizwa kwenye gari la polisi.Kigamboni (7) 
Baada ya kuwekwa kwenye gari.20160420_132851Ndugu wa marehemu Nice akienda kutambua mwili wa nduguye.Kigamboni (10)Gari la polisi lenye mwili wa marehemu likiondoka eneop la tukio.1
Mwili wa marehemu Daniel ulivyookolewa mapema asubuhi ya leo.
Kigamboni (11)Mratibu Idara ya Zima Moto, Brighton Monyo akielezea namna ambavyo miili hiyo ilivyookolewa.
WATU wawili waliofariki dunia alfajiri ya leo baada ya gari aina ya Toyota Hiace namba T271 CRG kuserereka wakati likiingia katika kivuko cha feri (ambacho kimekuwa kikitumika miaka yote) na kutumbukia baharini eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam. 

Waliofariki kutokana na ajali hiyo ni; Dereva la gari hilo mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Daniel (anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-35) mkazi wa Dar es Salaam ambaye aliokolewa saa tatu asubuhi ya leo na mwingine ni mwanamke aliyetambulika kwa jina la Nice Mwakalinga mwenye umri wa miaka 52 mkazi wa Tukuyu Masoko mkoani Mbeya. 

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu hao, marehemu Daniel ameacha mtoto mmoja na marehemu Nice ameacha watoto watano. 
Tayari miili ya marehemu wote imepatikana na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili taratibu zingine za mazishi zifanyike. 

Kaka ambaye ni manusura wa ajali hiyo anasema, ndugu hao waliotumbukia kwenye gari akiwemo dada yake Nice kwa pamoja walikuwa wakitokea mkoani Mbeya kwenye msiba. 
Tukio hili limetokea ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais john Pombe Magufuli kuzindua daraja jipya la Kigamboni (Nyerere Bridge) ambalo linatumika kwa ajili ya magari, waenda kwa miguu na baiskeli. 

Mashuhuda wa tukio wanasemaje? 
Kwa mujibu wa mmoja wa shuhuda alisema; 
“Dereva wa gari (Hiace) alikuwa akitokea kwenye ruti za usiku hivyo akawa anarudi nyumbani (Kigamboni) kupumzika lakini akiwa ndani ya gari (gari likiwa limeshaingia kwenye pantoni) alikuja mama mmoja ambaye alidai anajisikia vibaya kwani wametoka safari ya mbali (Mbeya) kuzika hivyo akaomba nafasi ya kupumzika ndani ya gari la dereva huyo. 

“Baada ya kuingia, yule dereva alipitiwa na usingizi kwa kuwa alikuwa amefanya kazi ya kuendesha gari usiku kucha. Wakati huo gari lake likiwa sailensa na pantoni likiwa limeshaanza kuondoka ndipo akajisahau na kukanyaga eksereleta na bahati mbaya kwa kuwa mnyororo wa kuzuia magari haukufungwa gari likaanza kutembea hadi kutumbukia baharini na kusababisha vifo hivyo.” 

Watumiaji wa kivuko hicho wanasemaje? 
“Tunamshukuru Rais Magufuli kutufungulia kivuko kipya (Nyerere Bridge) ila bado elimu zaidi inahitajika ili watu watumie hiki kivuko kipya japo kwa sasa kivuko cha zamani kinaonekana kuwa na magari machache lakini watu wengi wanaendelea kupanda pantoni. Mi nadhani endapo wengi wakitumia kivuko kipya itasaidia sana kuepukana na ajali kama hizi ambazo zinaweza kuepukika,” alisema mmoja wa watumiaji wa kivuko hicho. 

Naye Juma Khamisi ambaye ni mfanyabiashara katika eneo hilo, alisema; 
“Binafsi sifahamu kwa nini hawa jamaa (waliopata ajali) waliamua kutumia kivuko hiki ilihali kuna kivuko kipya ambacho ndiyo kwanza kina siku moja tangu kuzinduliwa kwake.” 
Kivuko hiki cha zamani (cha pantoni), kimekuwa na historia ya kusababisha ajali kama hizi mara kwa mara hivyo watu wanashauriwa kutumia kivuko kipya ili kuepusha ajali zinazoweza kuhatarisha maisha ya
Previous
Next Post »