RAIS WA NIGERIA BUHARI AFANYA ZIARA CHINA. - Rhevan Media

RAIS WA NIGERIA BUHARI AFANYA ZIARA CHINA.

Image copyrightAFP
Image captionRais Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anafanya ziara nchini China ambapo anatarajiwa kutia sahihi mikataba kadha ya kibiashara na uwekezaji baadaye wiki hii.
Pia bwana Buhari anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa China Xi Jinping.
Tangu achukue hatamu za uongozi mwaka uliopita, kiongozi huyo wa Nigeria amekuwa akifanya ziara kujaribu kuinua uchumi wa nchi hiyo ambao umeathirika kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.
Image copyrightAFP
Image captionUchumi wa Nigeria umeathirika kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.
Wajibu wa rais Buhari nchini China ni kupata mikopo ya kuziba pengo la dola milioni 10 katika bajeti yake.
Anataka kutumia pesa hizo kuboresha miundo msingi ya nchi hiyo iliyochakaa na kuwekeza kwenye kilimo.
Previous
Next Post »